Mchezaji wa zamani wa Simba ambae amevunja mkataba na klabu yake ya SonderjyiskE ya Nchini Denmark amesajiliwa katika klabu yake ya zamani ya S. C Villa kwa mkataba wa muda mfupi mpaka pale msimu wa mwaka 2016/2017 utakapomalizika.
Okwi aliyehusishwa na kurejea Simba na hatimae kunyakuliwa na S. C villa alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na SonderjyiskE baada ya kuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Mganda huyo aliuzwa na klabu yake ya Simba kwa klabu hiyo ya Denmark kwa dau nono lakini bahati mbaya hakuweza kuridhisha benchi la ufundi la SonderjyiskE na kuamua kuvunja mkataba.

EmoticonEmoticon