Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amejitetea juu ya maamuzi yake ya kutomuanzisha Theo Walcott katika mechi yao dhidi ya Watford ambapo Arsenal walichezea kichapo cha magoli 2-1.
Theo Walcott
Pamoja na kuonyesha kiwango bora kwenye mechi dhidi ya Southampton na kufunga magoli matatu (hat trick) katika ushindi wa magoli 5-0, Wenger alimuanzisha benchi Walcott na kumuingiza kipindi cha pili kitendo kilichopandwa na washabiki wengi.
Akizungumza na waandishi wa habari Wenger alidai Walcott asingeweza kucheza dakika 90 mechi mbili mfululizo. Alisisitiza kuwa Walcott alicheza kipindi cha pili kwa kumtoa Giroud inakuwaje analaumiwa.
"Ukiangalia nyuma Walcott hakucheza wiki tano na nusu. Alikuwa anasumbuliwa na maumivu mpaka kufikia siku ya jumatatu. Hakuweza kufanya mazoezi na wenzake." Aliongea Wenger
"Tuna mechi tatu wiki hii, tunajua vizuri sana, msifikirie sisi ni wajinga katika kufanya maamuzi. Nafikiri yalikuwa ni maamuzi sahihi, ni maamuzi ya kawaida tu."
Arsenal ilifungwa na Watford hapo jana 2-1 na kujiwekea mazingira magumu ya kuwania taji la EPA.

EmoticonEmoticon