Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Afcon Nchini Gabon baada ya kuitoa timu ngumu ya Burkina Faso kwa changamoto ya mikwaju ya penati (4-3) baada ya kumaliza dakika 120 wakitoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1 magoli yaliyofungwa kipindi cha pili Misri wakitangulia kufunga dakika ya 66 kupitia kwa staa wake Muhamed Salah na kusawazishwa baada ya dakika saba kupitia kwa Bance.
Burkina Faco walionekana kuwa fiti zaidi baada ya kuwapeleka mchakamchaka Misri lakini walishindwa kumalizia mipira iliyokuwaikifika mara kwa mara langoni kwa Misri.
Sifa pekee zimuendee kipa mkongwe kuliko wote El Hedary ambae ameweka rekodi ya kucheza fainali hizo mara 7 huku akiwa na umri wa miaka 44mbaada ya kuokoa mikwaju miwili ya penati na kuipeleka Misri fainali.
Nusu fainali nyingine itachezwa kesho kwa kuikutanisha miamba miwili katika soka la Afrika Cameroon na Ghana.

EmoticonEmoticon