Klabu soka ya Simba imeingia katika majaribu baada ya kupokea taarifa ya daktari juu ya Afya ya beki wake kisiki Abdi Banda, katika taarifa hiyo Abdi Banda anatakiwa apumzike kwa muda wa siku kumi kuitibu misuli yake kutokana na maumicu aliyopata siku baada ya mchezo wao na Azam.
Taarifa hii si nzuri kwa wana Msimbazi kwani tayari Banda alishakuwa na maelewano mazuri na safu ya ulinzi ya Simba kiasi cha kuonekana kuziba pengo la Juuko vilivyo na sasa ataukosa mchezo dhidi ya majimaji Wikiendi hii mjini Songea.
Banda amegeuka lulu kwenye safu ya ulinzi ya Simba inayonolewa na Mcameroon, Joseph Omog alipata majeraha hayo ya misuli baada ya kufanya mazoezi magumu kwa kipindi cha miezi miwili ambapo sasa amewekwa nje kwa ajili ya kuifanya misuli hiyo iachie.
Banda amekiri kutokuwa sehemu ya timu hiyo inayojiandaa na mechi ya Majimaji baada ya kupewa siku za kupumzika kutokana na majeraha hayo ya misuli.
“Mimi nipo nyumbani nimepewa siku 10 za kupumzika kwa ajili ya kupoza misuli yangu ambayo ilikaza baada ya kufanya mazoezi magumu kwa miezi miwili mfululizo na nitakosa mechi hii inayokuja dhidi ya Majimaji,”alisema Banda

EmoticonEmoticon