Shiza Kichuya ameongeza wigo wa magoli baada ya leo kuipa goli pekee na la ushindi klabu yake ya Simba kwa mkwaju wa penati dhidi ya Stand united katika mchezo uliochezwa katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga katika mchezo ulioisha kwa simba kushinda goli 1-0.
Mchezo huo uliokuwa mgumu muda wote kwa kuwepo kwa mashambulizi ya pande zote mara kwa mara kiasi cha kuleta presha wakati wote kwa mabenchi ya ufundi.
Simba walipata penati dakika ya 31 baada ya Laudit Mavugo kudondoshwa katika eneo la 18 la Stand United na kukwamishwa wavuni na Shiza Kichuya anayeongoza katika chati ya ufungaji wa magoli akiwa tayari na magoli 9 akifuatiwa na Tambwe mwenye magoli 7.
Kwa matokeo hayo Simba bado inaongoza ligi kwa kujikusanyia alama 35 ikicheza michezo 13 bila ya kupoteza hata mmoja.

EmoticonEmoticon