Timu ya Mbeya City leo imeutumia vizuri uwanja wake wa Nyumbani baada ya kushinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Yanga katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Goli la mapema kabisa lililofingwa kiustadi na Hassan Mwasapili mnamo dakika ya 6 tu ya mchezo kwa mkwaju wa faulo ambayo ilikwenda moja kwa moja na kumshinda Deogratius Munishi na kutinga wavuni.
Goli hilo liliamsha ari kwa upande wa Mbeya City walioonekana kuukamia mchezo huo na kulisakama lango la Yanga vilivyo walifanikiwa kupata goli la pili katika dakika ya 45 kupitia kwa Kenny Ally baada ya kucheza mpira wa faulo haraka haraka huku mabeki wa Yanga wakiwa wamezubaa na mnamo dakika ya 44 Donald Ngoma aliifungia Yanga goli la kufutia machozi, mpaka mpira unamalizika Mbeya City 2-1 Yanga.
Kwa matokeo hayo Yanga wanaendelea kubaki katika nafasi yao ya 2 na alama zao 27 wakiwa tayari wameshacheza michezo 23.
Wakati huohuo Mbeya City wanachupa mpaka nafasi ya 6 na alama zao 19.


EmoticonEmoticon