Timu ya Azam Fc imefungua usajili wake wa dirisha dogo kwa kishindo baada ya kuwasainisha wachezaji wawili raia wa Ghana Samuel Afful na Abdul Mohamed wote wakiwa ni washambuliaji.
Wakati Samuel Afful ilimlazimu apitie katika zoezi la majaribio na kufuzu Abdul Mohamed yeye amesajiliwa moja kwa moja kutokana na CV yake katika ligi ya Ghana.
Afful mchezaji kutika timu ya Sekondi Hasaacan ya Ghana Abdul ametokea katika klabu ya Aduana Stars akiwa mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo msimu uliopita
Afful amepewa miaka mitatu na Abdul amepewa mkataba wa miaka miwili.


EmoticonEmoticon