Na mwandishi wetu
Soko kuu la Mkoa wa Morogoro ambalo limdumu kwa Takribani miaka 73 tangia kujengwa kwake mwaka 1953, limeanza kubomolewa kupisha ujenzi wa soko jipya na la kisasa.
Jicho la Habari Tz, limeshuhudia ubomoaji wa soko hilo huku wafanyabiashara wakiendelea kutoa masalia ya vibanda vyao kama mabati na Mbao ili kwenda kuwasitiri sehemu nyingine.
Kwa mujibu wa msemaji katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro wafanyabiashara hao wamehamishiwa kwa muda katika maeneo ya Nanenane na Manzese ili kupisha ujenzi huo na pindi utakapokamilika basi watakodishiwa nafasi katika maeneo mbalimbali ya soko hilo linalotarajiwa kuanza ujenzi rasmi siku chache zijazo.




EmoticonEmoticon