Manchester United imeendelea kuchechemea katika ligi ya Uingereza baada ya leo kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Stoke City katika uwanja wa Old Tranford.
Goli la mapema la kipindi cha pili lililofungwa na Anthony Martial lilizimwa na lile la kusawazisha kwa upande wa Stoke City lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool Joel Allen katika dakika ya 83 ya mchezo.
Joe Allen akishangilia goli lake
Kwa matokeo hayo Manchester nasogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu Uingereza juu ya Chelsea.



EmoticonEmoticon