Serikali| Simba na Yanga marufuku uwanja wa Taifa

6:43 AM
Serikali imepiga marufuku watani wa jadi Yanga na Simba kuutumia Uwanja wa Taifa na zimetakiwa kutafuta viwanja vya kutumia.

Tamko hilo limetolewa na Serikali hivi punde baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kulieleza hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Uwanja huu sasa hautatumika na Yanga na Simba, hawawezi kufanya uharibifu huu wa makusudi huku wakijua kwamba uwanja huu ndani yake kuna kodi za walipa kodi.

“Mmeona walichofanya na sasa wanaweza kutafuta sehemu ya kwenda kucheza, watafute uwanja wa kutumia, hadi hapo tutakapoamua vinginevyo,” alisema Nape.

"Wanaotakiwa kuutumia ni ukiwa mzuri na si kama ulivyo sasa, wako wengine wastaarabu wanaweza kuutumia."

Mashabiki wa Simba waling'oa viti na kuvirusha uwanjani baada ya Amissi Tambwe wa Yanga kufunga bao na kabla ya kufunga alikuwa ameshika lakini mwamuzi hakuchukua uamuzi wowote.

Lakini mashabiki wa Yanga nao wakajibu mapigo ya kurusha viti baada ya Simba kusawazisha bao katika dakika ya 87 kupitia Shiza Kichuya.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »