Kamati ya bodi ya ligi kupitia kikao chake kilichofanyika jana oktoba 4 ,2016 imempia faini msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametozwa Faini ya shilingi laki 2 kwa kosa la kuingia uwanjani baada ya mechi baina ya Yanga na Simba kumalizika wakati yeye hakuwa miongoni mwa maofisa wa mechi waliotakiwa kuwemo uwanjani humo.
Adhabu ya Mananra ni kwa mujibu wa kanuni ya 14(10) Eneo husika ni kwa ajili ya wachezaji, mabenchi ya ufundi,wamuzi, madaktari,watoa huduma ya kwanza, wapiga picha na maofisa wengine wa mechi.
wakati huohuo kamati ya bodi ya ligi kupitia kikao chake hicho imeipiga faini ya shilingi milioni 3 klabu ya Azam fc kutokana na kuvaa beji ya mdhamini mkuu wa ligi mkono mmoja badala ya mikono miwili ambapo ni kinyume cha kanuni 13(1) na adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni 13(6)


EmoticonEmoticon