Kamati ya bodi na usimamizi wa ligi iliyoketi kwa masaa 72 kujadili matukio mbalimbali yaliyotokea katika mchezo baina ya Yanga na Simba na kutoa maamuzi ya kuipiga faini klabu ya Simba kwa vurugu zilizotokea katika mchezo huo pamoja na adhabu nyingine ilizozihushisha klabu za Azam, JKT Ruvu na Haji Manara.
Bodi hiyo imeshindwa kutoa maamuzi kwa marefa waliochezesha mchezo huo na walioonekana kushindwa kuendana na kasi ya mchezo huo na kushindwa kabisa kuumudu. Kamati hiyo imesema inaendelea kuupitia mkanda wa mechi hiyo ili kuweza kubaini makosa ya waamuzi yaliyojitokeza katika mchezo huo ili waweze kutenda haki katika maamuzi yao.
Hivyo basi Saanya na wenzake wataendelea na majukumu yao mpaka hapo bodi itakapotoa tamko rasmi la nini kimeamuliwa juu yao.

EmoticonEmoticon