TFF YAZISISITIZA YANGA NA SIMBA KUMALIZANA WENYEWE JUU YA ISHU YA KESSY

2:46 AM
 Hassan Kessy
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji imetoa siku tatu kuanzia Septemba 24, 2016 kwa viongozi wa klabu za Simba SC na Yanga SC kukaa chini na kumaliza suala la usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kwa njia ya mazungumzo ya kuelewana.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu kesi mbili zilizofunguliwa na Simba mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Richard Sinamtwa. Kesi ya kwanza iliyofunguliwa na Simba SC ni dhidi ya Yanga kudaiwa kuingia mkataba na mchezaji Hassan Kessy wakati bado ana mkataba na Simba SC.

Kesi ya pili ni Simba SC dhidi ya mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kudaiwa kuanza kufanya mazoezi pia kusajili Yanga na kwenda nje ya nchi wakati akiwa ndani ya mkataba na Simba SC. 

Kama hawatafikia mwafaka katika siku tatu walizopewa, mashauri hayo yatarudi mbele ya kamati na kufanya uamuzi kwa mujibu wataratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu Tanzania. Kupitia madai hayo, Simba inataka kulipwa dola 600,000 za Marekani.

Wakati huo huo, kamati imeondoa kifungo cha mwaka mmoja kwa mchezaji George Mpole wa Majimaji ya Songea baada ya klabu hiyo yenye maskani yake Mkoa wa Ruvuma kufikia mwafaka Kimondo FC. 

Pia kamati iliridhia mchezaji Enyina Darlington kutoka Nigeria kuanza kuitumika klabu yake baada ya kukamilisha vibali vya ukazi na kufanya kazi nchini vinavyotolewa na Idara ya Uhamiaji nchini katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »