Timu za Arsenal na Fc Basel leo usiku wanakutana katika dimba la Emirates katika mchuano wa klabu bingwa barani Ulaya
Mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na msisimko wa aina yake kutokana rekodi nzuri ya FC Basel dhidi ya timu za Uingereza,pia ikichagizwa na kasi ya hivi karibuni ya timu ya Arsenal kwenye ligi ya EPL hasa baada ya kuwanyuka mahasimu wao Chelsea mabao 3-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.
mchezo huo utawakutanisha ndugu wawili wa damu Granit Xhaka anayekipiga Arsenal na Taulant Xhaka anayekipiga Basel ambao wanatarajiwa kuongeza msisimko katika mchezo huo.
Vijana hawa waliwahi kucheza pamoja kwenye akademi ya Basel wakati wakiwa wadogo kabisa lakini leo hii wanaenda kukutana wakiwa wakubwa na kila mmoja akicheza timu nyingine.
Hii si mara ya kwanza kwa wawili hawa kukutana kwani awali walikutana kwenye Michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa, Granit akichezea Uswisi na Taulant akichezea Albania

EmoticonEmoticon