Timu ya Borussia Dortmund jana usiku imeikatalia Timu ya Real Madrid baada ya kuchomoa goli dakika za lala salama za mchezo huo wa klabu bingwa barani Ulaya uliokuwa wa kukatana shoka.
Ilibidi kuwasubiri mpaka dakika ya 87 ya mchezo huo kuchomoa goli la pili ambapo Madrid alikuwa akiongoza kwa magoli 2-1,
Shukrani pekee zimuendee mchezaji wa zamani wa Chelsea anaekipiga Dortmund Andre Schuerrle kwa kusawazisha goli hilo.
Awali Christiano Ronaldo alitangulia kufunga goli la kwanza katika dakika ya 17 ya mchezo huo kabla ya kusawazishwa na Aubameyang dakika ya 43.
Varane aliipatia Madrid goli la pili dakika ya 63 lililosawazishwa na Schuerrle dakika ya 87 ya mchezo. hadi filimbi ya mwisho inapulizwa matokeo yalikuwa 2-2.
Kama uliikosa mechi hiyo unaweza kuitazama hapo chini.




EmoticonEmoticon