MAVUGO ATOA YA MOYONI JUU YA LIGI YA BONGO

1:45 AM
Mahambuliaji wa Timu ya Simba Laudit Mavugo aliyeifungia timu hiyo mabao matatu kwenye mechi nne, ametamka kwamba ushindani wa ligi hiyo ni mkubwa zaidi ya aliokuwa anakutana nao nchini kwao Burundi, ambapo mabeki wengi wamekuwa wakicheza zaidi ya kazi ili kulinda timu yao isifungwe.


Straika huyo wa zamani wa Vital’O ya Burundi ameliambia Championi Ijumaa, kwamba wapinzani wao hasa mabeki, wamekuwa wakiwafanyia vitendo visivyo vya kimichezo ili kuwaondoa katika hali ya kimchezo na pia wasipate nafasi ya kufunga mabao.

“Bongo mambo ni magumu kwa sababu wapinzani mara nyingi wanatufanyia vitendo ambavyo ni vya kukera na visivyo vya kimpira kwa lengo tu watuondoe katika hali ya kiuchezaji lakini pia hiyo ikiwa ni mbinu ya wao kujilinda.

“Lakini kwangu wala sijali na badala yake nitaendelea kupambana zaidi na zaidi kuitetea timu yangu kuhakikisha inaibuka na ushindi katika kila pambano,” alisema Mavugo.


SOURCE: CHAMPIONI

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »