FOSTER- TUNANGOJA AMRI YA KUUZA MALI ZA MBOWE

2:09 AM
KAMPUNI ya Udalali ya Fosters Auctionare imesema bado Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) halijawapa taarifa zaidi kuhusu kuuza mali zilizokuwa katika ofisi za Kampuni ya Freemedia katika jengo lililokuwa limepangishwa na Freeman Mbowe akidaiwa Sh bilioni 1.172.

Ofisi hizo zilitumika kwa uchapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na ukumbi wa disko wa Billicanas ambao Septemba mosi, madalali hao wakiwa na watumishi wa Kitengo cha Madeni cha NHC walitoa samani mbalimbali pamoja na vifaa vilivyokuwamo na kuvitoa nje.

Samani za kampuni ya Free Media inayomilikiwa na Freeman Mbowe zikiwa nje ya jengo lenye ofisi za kampuni hiyo baada ya kampuni ya udalali ya Fosters kuzitoa kwa nguvu nje ya ofisi kwa madai ya kudaiwa kodi ya jengo na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dar es Salaam jana. (Picha na Fadhili Akida).

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joshua Mwaituka alisema leo ndio siku 14 zinaisha tangu walipochukua mali hizo, lakini hawajapata idhini kutoka NHC juu ya kuuza mali hizo.

“Kwa utaratibu kampuni inapomaliza kukusanya mali za mdaiwa, huzihifadhi katika ghala letu lililopo Buguruni na ndani ya siku 14 huviuza, ikiwa tutakuwa tumepata idhini kutoka kwa mamlaka husika,” alisema Mwaituka na kuongeza kuwa NHC bado wako kimya.

Hata hivyo, alisema amepata taarifa kutoka vyombo vya habari kuwa lipo zuio la Mahakama kuhusu uuzwaji wa mali hizo, lakini NHC haijawasiliana naye kumpa taarifa zaidi.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »