Leo ni siku ya 5 Tangu wiki ya Simba Day kuanza ambapo siku ya saba itahitimishwa na mpambano wa kirafiki pale uwanja wa Taifa baina ya Simba na AFC Leopard ya Kenya sambamba na utambulisho wa kikosi cha simba kitakachoshiriki ligi kuu msimu ujao, Tayari Simba imeshawapa mikataba wachezaji wake wanne wa kigeni waliokuwa katika majaribio ambao ni Janvier Besala Bokungu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, kiungo Mussa Ndusha kutoka DRC pia na washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast pamoja na kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Burundi Laudit Mavugo.
Ikiwa ni siku ya 5, klabu ya Simba inaitumia siku hii kufanya usafi katika mtaa wao wa Msimbazi maeneo ya kariakoo wakiishia kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo viongozi na wanachama wa klabu hiyo wamejitokeza kushiriki zoezi hilo wakiongozwa na mgeni rasmi Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu.

EmoticonEmoticon