Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Hispania La Liga Javier Tebas ameonyesha hofu yake ya kuondokewa na mchezaji wa Dunia katika ligi kuu ya Hispania anaekipiga katika klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Kitendo cha Messi na baba yake kupatikana na hatia ya udanganyifu wa kulipa kodi na kuhukumiwa miezi 21 jela lakini ataendelea kucheza soka huku kifungo hicho kinaendelea iwapo atalipa faini ya pauni milioni 1.7 kinaonekana kumkera Messi ambae anaamini hana hatia na tayari amekwishakata rufaa.
Tayari Rais wa klabu ya Barcelona ameshatangaza hadharani kwamba wapo bega kwa bega na mwanasoka huyo dhidi ya kesi yake na kuondoa uvumi kwamba klabu hiyo imemtelekeza.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania Messi atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi chote hicho cha miezi 21 na endapo atapatikana na kosa jingine basi hukumu yake ni kwenda gerezani moja kwa moja hali inayoleta mashaka kwa Messi kuendelea kubaki nchini humo.
Tayari klabu za Manchester City na Barcelona zimetwajwa kumuwinda gwiji huyo wa soka Duniani na wanaonekana kutaka kuutumia huu mwanya kuweza kumshawishi Messi kuhama Catalunya.




EmoticonEmoticon