MWANADADA anayefanya vyema kwenye Tasnia ya Mitindo Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa katika ulimwengu wa siasa hakuna kitu anachokizimia kama spidi ya kuongoza na kubadilisha baadhi ya mambo nchini aliyonayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Jokate aliongeza kuwa Magufuli amekuwa mkombozi katika taifa hili, kwake ni kiongozi bora ambaye anatazamia kulinusuru taifa katika dimbwi la umaskini. Jokate aliongeza kuwa jambo ambalo anapenda kumshauri mheshimiwa ni kuhakikisha nguvu zake si za soda, apambane katika mwendo huo mpaka mwisho.
“Mimi ni muumini wa siasa kwa sasa na siku moja natarajia kujiingiza huko, sasa kati ya vitu vinavyonivutia ni namna ambavyo rais wetu anajitahidi kutumbua majipu kwa kila namna huku akihakikisha nidhamu inakuwepo serikalini. Ni kitu kizuri sana anachofanya pia ninamuombea kwa Mungu aendelee na moyo huohuo,” alimaliza Jokate.
GPL

EmoticonEmoticon