Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga, leo imefanikiwa kuendelea kujikita kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya Stand United kutoka mjini Shinyanga.
ANGALIA MAGOLI KATIKA VIDEO HAPO CHINI
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Taifa umeshuhudia Simon Msuva akikamata usukani wa ligi kwa mara ya kwanza baada ya kufunga goli moja na kufikisha idadi ya magoli kumi na kumuacha shida kichuna aliyeshikilia usukani huo kwa kipindi kirefu.
Magoli ya Yanga leo hii yamefungwa na Donald Ngoma dk 17, la pili likipachikwa na Msuva dk 27,Obrey Chirwa akafunga goli la 3 dk 52, Nadir Haroub akamalizia kwa kupachika goli la 4 dk 68.
Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kujitanua kileleni kwa kujikusanyia alama 49 huku ikiwapa mtihani watani wao Simba ambao wanashika nafasi ya pili na alama zao 45 Wakitarajia kushuka dimbani kesho mjini Songea kukipiga na Timu ya Majimaji ya mjini humo.


EmoticonEmoticon