
Lampard ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni katika klabu ya New York City FC amesema hataongeza tena mkataba na wala hatosajili kwenye timu yoyote japo timu nyingi zimeonyesha nia ya kumuhitaji.
Lampard amesema kwa sasa soka basi na anafungua ukurasa mpya wa maisha.
Lampard ameitumikia Timu ya Taifa ya Uingereza kwa kuichezea mechi 106 ataenda kuaga katika klabu za Westham united, Manchester City na mwisho Chelsea klabu ambayo ameichezea kwa miaka 13.
Lampard mwenye umri wa miaka 38 amesema hatoweza kuisahau timu ya Chelsea kwa kumpa mafanikio makubwa kisoka.
EmoticonEmoticon