Timu ya Yanga leo imeivurumushia bila huruma Timu ya Ndanda kwa jumla ya magoli 4-0 katika mchezo uliomalizika punde katika dimba la uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kupunguza pengo la pointi dhidi ya Simba, Yanga imefikisha pointi 40 huku Simba wakiwa juu na pointi zao 41 wakizidiwa mchezo mmoja na Yanga na watashuka dimbani kesho dhidi ya Ruvu shooting.
Katika mchezo wa leo Yanga walianza kujipatia goli katika dakika ya 4 tu ya mchezo kupitia kwa Donald Ngoma na kuongeza goli la pili dakika chache baadae huku Amis Tambwe akipachika goli la 3 kabla ya mapumziko.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana
Mpaka timu zinakwenda mapumziko Yanga ilikuwa mmbele kwa magoli 3-0 dhidi ya Ndanda.Kipindi cha pili kilianza kwa kupooza huku Yanga wakionekana kurelax zaidi na kuchezea mpira muda mwingi mpaka ilipofika dakika ya 89 beki wa Yanga Vicent Bossuo alipoweza kuifungia Yanga goli la 4 kwa kichwa akiungonisha mpira wa kona uliopigwa na Juma Abdul.
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa;
Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Said Juma ‘Makapu’/Justine Zulu dk60, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Thabani Kamusoko dk70, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk77.
Ndanda FC;
Jeremiha Kisubi, Kiggi Makassy, Bakari Mtama, Paul Ngalema, Hemed Khoja, Salvatory Ntebe/Ayoub Shaaban dk40, Abuu Ubwa/Salum Minely dk53, Nassor Kapaman Salum Telela, Omar Mponda na Riffat Khamis.
VIDEO YANGA VS NDANDA 4-0



EmoticonEmoticon