TETESI| KOCHA WA TP MAZEMBE KUJA KUIFUNDISHA AZAM FC

10:11 PM
Aliyewahi kuwa Kocha wa TP Mazembe Lamine N'Diaye anaweza kutua Azam Fc wakati wowote kimeripoti chanzo kimoja cha habari hapa nchini.
N'Diaye raia wa Senegal ambaye aliwahi kukipiga katika kikosi cha Cannes ya Ufaransa, ni kati ya makocha wanaopewa nafasi ya kuinoa Azam FC.

“Kweli kuna ishu ya Kali (Ongala). Anaweza kuanza kazi na timu halafu wakikubaliana na N'Diaye, basi anakuja kuwa bosi.

“Unajua ni kocha mkubwa, Mazembe amekuwa hadi mkurugenzi wa ufundi. Ni mtu mtaalamu sana na soka la Afrika, usisahau aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Senegal,” kilieleza chanzo.
N'Diaye aliisaidia Mazembe kuchukua makombe ya ubingwa wa Congo na makombe mengine, ubingwa wa Afrika kuanzia akiwa kocha na baadaye mkurugenzi wa ufundi.

Azam FC imetangaza kumtimua Kocha Zeben Hernandez na makocha wasaidizi wote.

N'Diaye alitua TP Mazembe mwaka 2010, baadaye mwaka 2013 akawa mkurugenzi wa ufundi. Lakini amewahi kufundisha timu ya taifa ya Senegal.

Kabla aliifundisha Coton Sport ya Cameroon kwa mafanikio pia Maghreb Fez ya Morocco.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »