Timu ya Simba imefanikiwa kuongeza wigo wa alama kileleni baada ya leo kujikusanyia alama tatu muhimu kwa kuifunga timu ya Ruvu shooting na kufanikiwa kufikisha alama 44 wakiwaacha watani wao Yanga na alama zao 41.
Goli la Simba lilipachikwa katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Muhamed Ibrahim maarufu kama 'Mo'
Baada ya ushindi huo Simba inataraji kuondoka kesho kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya mapinduzi.


EmoticonEmoticon