Goli 1 la John Rafael Bocco limeipa ushindi Timu ya Azam fc dhidi ya wageni wao Timu ya Prison.
Azam Fc imeingia katika mchezo huo huku wakiongozwa na mwalimu Nasoro Idd Cheche baada ya kufukuza benchi zima la ufundi lililoongozwa na Muhispania Hernandez. Azam waliuanza mchezo kwa kasi huku washambuliaji wa Azam wakikosa magoli mara kwa mara.
Katika mchezo huo kiungo wa Prison Kazungu Mashauri alipewa kadi nyekundu na kuwalazimu Prison kumaliza mchezo wakiwa pungufu.
Kwa matokeo hayo Azam fc wanasogea mpaka nafasi ya tatu wakiishusha Mtibwa na Kagera Sugar.

EmoticonEmoticon