WOLPER ANUNUA GARI YA MILIONI 20

8:58 AM

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper akiwa kapozi na gari hilo aina ya Toyota Alphard .

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 20 ambalo kwa sasa anamalizia usajili wake.
Muonekano wa ndani wa ndinga yake hiyo mpya.

Chanzo kilimbabatiza Wolper mitaa ya Kinondoni jijini Dar akiwa na gari hilo aina ya Toyota Alphard ambapo alipobanwa kama amelikodi kama wanavyofanya mastaa wengine au amenunua alifunguka kuwa ni lake kutoka kwenye hela yake halali.
Wolper akiwa katika pozi.

“Hii gari ni yangu kama mnavyoiona mpya kabisa, nimeinunua na ndo’ kwanza nashughulikia usajili,” alisema Wolper.

Wolper alisema kuwa anakwepa mambo yaliyompata kwenye ile gari yake iliyomletea matatizo aina ya BMW X-6 ambapo alipata funzo na sasa hawezi kufanya makosa tena.
Gari aina ya Toyota Alphard.

“Nimeamua nifanye usajili kabisa TRA, sitaki matatizo kabisa kuhusu magari, lile lilinifanya nipate funzo kubwa,” alisema Wolper.

Wolper mbali na kununua gari amefungua duka la nguo Kinondoni. Kufuatia mambo hayo makubwa aliyofanya msanii huyo, wadau walihoji kama mkwanja wa kufanyia yote hayo umetokana na safari ya China au kuna pedeshee kaamua kumpa maisha? Jibu analo mwenyewe.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »