Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Fredrik Sumaye amefutiwa hati miliki ya Shamba lake huko Bunju Jijini Dar es Salaam.
Shamba hilo linaloingia mikononi mwa Serikali, ni lile liliko katika eneo la Mwabwepande jijini Dar es Salaam ambalo mwishoni mwaka jana, wananchi waliobomolewa nyumba zao ikidaiwa walilivamia na kujenga.
Leo serikali imetangaza rasmi kufuta leseni ya eneo hilo.
Sumaye aliwahi kueleza kuwa ameliacha eneo kwani lengo lake ni kujenga chuo kikuu na sio vinginevyo. Aliweka wazi nia yake ya kufika mahakamani endapo atanyang’anywa eneo hilo.

EmoticonEmoticon