SAKATA LA KESSY, KIBAO CHAIGEUKIA SIMBA

5:32 PM
Klabu ya Simba imetakiwa kuwasilisha vithibitisho vya kumlipa mishahara beki wake, Hassan Ramadhan Kessy katika miezi mitatu ya mwisho kuelekea kumaliza mkataba wake.

Hiyo inafuatia hoja iliyowasilishwa na Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa leo katika kikao cha Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji kwamba Simba haina uhalali wa madai yoyote dhidi ya Kessy kwa sababu haikumlipa mishahara kwa miezi mitatu.

Kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam jana, Yanga walidai kwamba Simba hawakumlipa mchezaji huyo kwa miezi mitatu kuelekea mwisho wa Mkataba wake na kwa mujibu wa sharia hawana haki ya madai yoyote dhidi yake.

Habari za ndani kutoka kwenye kikao hicho chini ya Mwenyekiti wa Kamati, Wakili Richard Sinamtwa zinasema kwamba Katibu Mkuu wa Simba SC, Patrick Kahemele aliyeiwakilisha klabu yake leo, ametakiwa kuwa amewasilisha vithibitisho hivyo kesho.

Yanga waliiomba Kamati ipokee vithibitisho vya vielelezo vya kupelekwa mishahara ya Kessy kwenye akaunti yake ya benki na si vinginevyo – kwa kuwa wana wasiwasi wapinzani wao wanaweza kufoji nakala za kumlipa mkononi. 

Simba inalalamikia klabu ya Yanga kumsajili beki Kessy akiwa hajamaliza mkataba wake Msimbazi na kwa sababu hiyo inataka kulipwa Sh. Milioni 200 ambayo ni punguzo kutoka Bilioni 1.2 walizotaka awali.








Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »