Beki wa Ynaga Juma Abdul huenda akakosekana kipindi chote kilichobaki kuelekea kualizika kwa mwaka 2016 kutokana na maumivu ya nyonga yanayomsumbua.
Kwa mujibu wa Daktari wa timu hiyo Edward Bavu, amesema Juma yupo chini ya uangalizi maalum ili kuhakikisha napata matibabu stahiki na kurejea mapema zaidi uwanjani.
“Kwa sasa tunaangalia maendeleo yake kabla ya kurudi uwanjani rasmi, kama akionekana bado ataendelea kukaa nje mpaka pale tutakaporidhika juu ya afya yake,” alisema Bavu.
Hata hivyo pamoja na daktari huyo kusema hivyo kumekuwa na hofu kubwa kuwa beki huyo hataweza kurudi uwanjani hadi Januari mwakani, kutokana na mechi tatu zilizobaki za mzunguko wa kwanza kuwa karibukaribu.
Yanga wanacheza na Mbeya City, halafu watavaana na Mbeya City wikiendi ijayo na mwisho watamaliza na Ruvu Shooting.
Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kumalizika Jumapili ijayo lakini viporo vitaenda hadi Novemba 13.

EmoticonEmoticon