Timu ya Geita District ya Geita imeshindwa kutokea katika Dimba la kaitaba kucheza na Mabingwa wa Mkoa wa Kagera timu ya Murusagamba kutoka Ngara katika michuano ya Azam federation Cup ambayo ipo katika hatua za awali.
Ilibidi waamuzi kuwasubiri kwa dakika 15 lakini timu ya Geita ilishindwa kutokea na ndipo mwamuzi wa pambano hilo alipopuliza kipenga kuashiria mchezo huo kumalizika.
Kwa mujibu wa kanuni za soka timu ya Murusagamba itapewa pointi 3 za mezani na magoli 2 na kusonga mbele katika michuano hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kabla ya kumalizika kwa pambano hilo iliripotiwa Timu ya Geita ilipata tatizo la kiusafiri wakiwa njiani kuelekea kwenye mpambano huo.

EmoticonEmoticon