Na Ripota wetu. Dsm
Timu za Simba na Yanga leo zimemaliza ubishi uliobishwa takribani wiki nzima kuelekea pambano lao lilopigwa leo kunako uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuishia kwa matokeo ya 1-1
Walikuwa ni Yanga walioanza kuliona goli la Simba kupitia kwa mshambuliaji wao Amis Tambwe katika kipindi cha kwanza baada ya kumalizia pasi ndefu iliyopigwa na Mbuyu Twite.
Baada ya goli hilo ilizuka tafrani uwanjani wachezaji wa Simba wakionekana kulalamikia goli hilo ambalo lilionekana kwamba mfungaji aliunawa mpira kabla ya kufunga.
Tafrani hiyo ilisababisha kuonyeshwa kwa kadi nyekundu nahodha wa Timu ya Simba Jonas Mkude na kusababisha timu ya Simba kumosa maelewano na kutawaliwa na Yanga.
Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko ambapo Ajib, Lufunga na Mavugo walienda benchi na kuingia Juuko, Ibrahim na Blagnon, mabadiliko hayo yalileta uhai kwa upande wa Simba waliokuwa pungufu na kufanikiwa kusawazisha goli dakika ya 87 ya mchezo kupitia Shiza Kichya ambae linakua ni goli lake la 5 msimu huu na kufanikiwa kuongoza safu ya wafumaniaji nyavu.
Katika mchezo huo polisi iliwalazimu kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatuliza mashabiki wa Simba walioonekana kushikwa na jazba na kuanza kung'oa viti baada ya kufungwa goli la kwanza.
Hata hivyo hali ilitua na mpira ukaendelea na mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho Yanga 1-1 Simba





EmoticonEmoticon