Klabu ya Toto African ya Mwanza leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa magoli 2-0 dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar.
Ikicheza chini ya KOcha wake mpya Khalfan Ngasa Timu ya Toto ilipata magoli yake leo kupitia kwa Jaml Soud na Muhamed Soud.
Kwa matokeo hayo Toto inafikisha alama nane baada ya kucheza mechi nane, ikishinda mbili, sare mbilina kufungwa mechi 4.
Wakati huohuo Timu ya Stand United imelazimishwa sare ya 0-0 na Mbeya City na kushindwa kuwashusha kileleni Simba inayoongoza ligi kwa alama 17, ikifuatiwa na Toto yenye alama 16 baada ya sare ya leo.
EmoticonEmoticon