RC MAKONDA AMPA MILIONI 10 KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO| MADAKARI WASEMA HATOWEZA KUONA TENA

12:08 PM

SIKU chache mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kosa la kumtoboa macho ndugu, Said Ally wa Buguruni kwa Mnyamani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda ameamua kuendelea kumsaidia kijana huyo katika hatua zake zote za matibabu na mtaji wa Shilingi Milioni kumi.Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kijana huyo kufika katika ofis za mkoa.
Makonda alisema kuwa mara baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari Bingwa wa Muhimbili imeonekana kuwa bado Said hatoweza kupata tena nafasi ya kuona tena hivyo anahitaji matibabu ya ziada.“Serikali ya mkoa imetoa gari ambayo atatumia kwa kipindi chote akiwa anaenda kupatiwa matibabu na shughuli zingine ambazo atakuwa anafanya mpaka hapo atakapokuwa sawa”alisema Makonda.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Said Ally, ambaye ametobolewa macho na Mkewe Zara Sudi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandish wa Habari.
Kwa upande Ndugu Said Ally amesema kuwa anawashukuru madaktari kwa juhudi zote walizofanya na shukrani kubwa sana ziende kwa Gea Habibu wa Clouds Media na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa moyo wake aliounyesha kwa kujitoa kwa hali na mali.

“Kiukweli nimeona Mungu akiwa katika upande wangu kwa msaada ninaondelea kupata kutoka kwa mkuu wa Mkoa na watu wa Clouds na madakatari naomba mungu aweze kuwapa maisha marefu” alisema Said.

Makonda alimaliza kwa kusema kuwa Serikali ya mkoa inandaa utaratibu kwa ajili ya watu wengine ambao wanahitaji kujitolea kumsaidia Said hivyo jumatatu atatangaza rasmi.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »