SIMBA NA YANGA ZARUHUSIWA KUTUMIA UWANJA WA UHURU

10:29 PM

Bodi ya ligi Tanzania imethibitisha timu za Simba na Yanga zitautumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani baada ya serikali kuzizuia kuutumia uwanja wa taifa kama uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi zao za ligi kuu.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema, mechi ijayo ya Yanga wataanza kucheza kwenye uwanja huo dhidi ya Mtibwa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi October 13.

“Mechi zao watacheza kwenye uwanja wa Uhuru, kwahiyo mechi zao zote za nyumbani watakuwa wakitumia uwanja huo. Serikali ilizifungia kutumia uwanja wa taifa, uwanja wa Uhuru uko wazi wanaweza kuutumia wakati wowote,” anathibitisha Boniface Wambura.

Awali vilabu hivyo vilikuwa vinautumia uwanja huo kwa mechi zao za ligi kabla ya Simba kuulamimikia kuwa unawasababishia majeraha wachezaji wao na kuomba kurudishwa kwenye uwanja wa taifa.

Serikali ilichukua uamuzi wa kuufungia uwanja wa taifa kufatia vurugu za mashabiki zilizozuka kabla na wakati wa mchezo wa Yanga vs Simba uliochezwa October Mosi. Kabla ya mechi hiyo, mashabiki waling’oa mageti manne kabla ya mashabiki wa Simba kung’oa viti wakati mechi ikiendelea kwa madai klabu yao ilikuwa ikionewa katika mchezo huo

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »