Timu ya Simba imeendeleza rekodi yake ya kucheza mechi 12 bila ya kupoteza na kuzidi kujiimarisha kileleni.
kama ulidhani ni nguvu ya soda basi utakuwa unakosea, ikicheza kwa kujiamini kana kwamba ipo uwanja wa nyumbani timu ya Simba imeweza kuchomoza kwa magoli 3-0 dhidi ya wenyeji wao Mwadui katika mtanange uliopigwa katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Ibrahim Mo ambaye ndio alikuwa nyota wa mchezo wa leo aliweza kuifungia timu ya Simba magoli mawili katika kila kipindi huku mfungaji anayeongoza kwa sasa katika chati ya ufungaji bora Shiza Kichuya akifunga goli moja na kujikusanyia jumla ya magoli nane.
Kwa ushindi huo Simba sasa inafikisha pointi 32 ikicheza michezo 12 ya ligi.
Kwa ujumla Timu zote zilicheza kwa utulivu huku Mwadui wakikosa nafasi kadhaa za kufunga walizopata huku Simba wakitumia makosa ya mabeki wa Mwadui.
Katika mchezo huo mshambuliaji wa Simba Ludit Mavugo alitolewa mapema kipindi cha kwanza baada ya kuonekana kukosa magoli ya wazi na pengine kutofuata maagizo ya kocha kwa utimmilifu wake na nafasi yake kuchukuliwa na Ame Ali aliyetoa pasi ya goli la tatu.

EmoticonEmoticon