KUWA MAKIN..I!!! MATAPELI WAMEVAMIA UHAKIKI WA VYETI FEKI

1:10 AM
Wakati halmashauri mbalimbali nchini na Baraza la Mitihani (Necta) wakiendelea na uhakiki wa vyeti vya elimu kwa watumishi wa umma, matapeli nao wamepata mwanya wa kujipatia fedha kutoka kwa waliopoteza vyeti.

Ni kwamba, ili uhakikiwe na Necta kwamba uliwahi kusoma kwenye shule au chuo fulani cha elimu nchini au nje ya nchi lakini cheti chako kimepotea, kimeharibika au kimeungua, unatakiwa kuripoti polisi na kutangaza gazetini.

Na kutokana na 'utitiri' wa matangazo ya vyeti kupotea kwenye magazeti mbalimbali nchini tangu kutangazwa kwa uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, matapeli wametumia fursa hiyo kupata fedha kutoka kwa waliopoteza vyeti kwa kuwapigia na kuwaambia vyeti vyao wanavyo.

Akizungumza na Nipashe kwenye ofisi za Necta jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita, Ismail Kihaga, mwajiriwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieleza jinsi matapeli hao walivyotaka kujipatia fedha kutoka kwake.

Alisema kuwa baada ya kutangaza gazetini wiki iliyopita kuwa amepoteza baadhi ya vyeti vyake vya elimu ya sekondari na chuoni, alipigiwa simu na mtu ambaye alidai kuwa ndugu yake anavyo.

"Nilipotangaza kupotelewa na vyeti vyangu wiki hii, kuna jamaa alinipigia simu na kuniambia ameona tangazo langu na kuchukua namba zangu za simu na kudai kwamba vyeti vyangu viliokotwa na ndugu yake ambaye ni meja jeshini," alisema.

"Aliniambia kwamba ndugu yake huyo yuko jeshini mkoani Morogoro lakini kuna mtoto wake anasoma mjini Morogoro hivyo anaweza kumtuma avilete vyeti vyangu Dar es Salaam ikiwa nitampatia Sh. 20,000 ya nauli.

"Kwa jinsi alivyokuwa anazungumza, nikabaini anakosa kujiamini na nikahisi huenda akawa tapeli. Nilikata simu yake ili nijipange kwanza kujua cha kumuuliza na cha kufanya kama kweli vyeti vyangu anavyo.

"Baadaye nilipofakari na kujua cha kufanya, nikamwambia anipatie namba za simu za huyo ndugu yake ambaye kweli alidai vyeti vyangu vyote nilivyotangaza gazetini anavyo.

"Kwa sababu najua kuna matapeli na sikutaka kuwa sehemu ya watu wanaolizwa na matapeli hawa, nikamwambia ampatie huyo mtoto wake hiyo Sh. 20,000 waliyotaka, akiniletea nikawaahidi nitampa laki mbili (Sh. 200,000)."

Alisema alishtushwa na madai ya tapeli huyo kwamba vyeti vyake viliokotwa na meja wa jeshi mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwaka huu, ilhali vilipotea nyumbani kwake miaka mingi iliyopita na huenda alivichanganya kwenye maboksi ambayo familia yake iliyachoma moto.

Kumekuwa na matangazo mengi ya kupotea kwa vyeti vya kitaaluma tangu serikali ilipotangaza zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo kwa watumishi wa umma ili kuwabaini wenye vyeti feki.

Wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17 bungeni mjini Dodoma Mei 26, Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alitangaza kuanza kwa uhakiki wa vyeti vya elimu kwa watumishi wa umma.

Alisema serikali itawaondoa katika utumishi wa umma wale wote walioajiriwa wakitumia vyeti bandia.

Aliwataka watumishi wa aina hiyo kuanza kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kabla ya kufikiwa na mabadiliko ya kusafisha
Source ipp media

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »