Timu ya Manchester united leo imekiona cha mtemakuni Darajani, mbele ya klabu ya Chelsea baada ya kukumbana na kipgo cha magoli 4-0.
Hicho ni kipigo kibaya zaidi tangia kocha Jose Morinho kutua ndani ya klabu hiyo tajiri na yenye wapenzi wengi Duniani.
Walikuwa ni Chelsea waliokuwa katika dimba lao la Stanford Bridge, walipoanza kuiadhibu klabu ya Man u katika dakika ya kwanza tu ya mchezo pale Pedro alipokwamisha mpira wavuni na kuiandikia Chelsea goli la kwanza.
Beki wa kutumainiwa wa Chelsea Gary Cahill alifunga goli la pili kunako dakika ya 21 ya mchezo huo kabla ya E. Hazard kufunga goli la 3 dakika ya 62 huku Ngolo Kante akishindilia msumari wa mwisho katika dakika ya 70 ya mchezo huo.
Unaweza kuangalia magoli ya mechi hiyo hapo chini
ULIKOSA KUONA KICHEKESHO HIKI? BOFYA HAPO CHINI KUMUONA SALOME

EmoticonEmoticon