BONDIA THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA

11:14 PM
Habari zilizotufikia punde zinasema Bondia Thomas Mashali amefariki Dunia,
Taarifa zinaeleza Mashali ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuokotwa vichakani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »