Azam Fc imefanikiwa kujikusanyia pointi tatu muhimu baada ya kupata ushindi wa ugenini wa magoli 3-2 dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa leo katika dimba la Kaitaba.
Walikuwa Kagera Sugar waliotangulia kujipatia goli katika dakika ya 33 kupitia kwa mshambuliaji wake Themi Felix, Azam walicharuka na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 40 goli likifungwa na kiungo mshambuliaji Mudathir Yahaya. Mpaka Timu zinakwenda mapumziko magoli yalikuwa ni 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini walikuwa Kagera Sugar tena waliotangulia kwa kufunga goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wake yuleyule Themi Felix aliyefunga goli dakika ya 68,
Iliwalazimu Azam kusubiri mpaka dakika ya 81 kuweza kusawazisha goli hilo kupitia kwa Frank Domayo kabla ya nahodha wa Azam Jonh Bocco kuifungia Azam goli la Tatu na la ushindi katika dakika ya 86.

EmoticonEmoticon