MREMA ANENA| MAANDAMANO YANAONGEZA WAFUNGWA MAGEREZANI

8:15 AM




Dar es salaam. Mwenyekiti Bodi ya Parole ,Augustine Mrema amesema maandamano ni uhaini na chanzo kinachotengeneza wafungwa watarajiwa nchini. 

Mrema amesema hayo leo kupitia mkutano wake na Kamishna Mkuu wa Magereza nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

"Haiwezekani inji(nchi) hii ikiwa ya maandamano tu.Enzi ya rais Kenyatta ilikuwa hata ukifikiria tu kwamba atakufa lini ,tayari unakuwa umefanya kosa kisheria, sasa hautaki au unataka Rais ni Magufuli ,sasa wasisababishe ongezeko la wafungwa watarajiwa ndiyo maana nilizungumza na bodaboda na wale dada poa pale uwanja wa fisi ili kupunguza kasi ya wafungwa watarajiwa,"alisema.

Pia ameagiza Jeshi la Magereza nchini kutoridhika na manufaa ya wafungwa kupitia ya sheria ya Parole na bad ala yake ifanyiwe maboresho ili kusaidia kupungua kwa wafungwa wengi gerezani. 

Sheria ya Parole ya 1994 ilifanyiwa maboresho yake mwaka 2002 katika kifungu change 4 na kupungua idadi miaka kutoka minane hadi minne kwa mfunguwa anayetakiwa kunufaika na Parole.
Source:Mwananchi

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »