Ni siku tano tu zimepita tangia vijana watano wapandishwe kizimbani baada ya kudhalilisha Rais Magufuli pamoja na kulitusi jeshi la Polisi katika mitandao ya Facebook na Whatsapp, jana kijana mmoja ambae ni mfanyabiashara anaefahamika kwa jina la Christon Mbalamula (28) amefikishwa amefikishwa katika mahakama ya Kisutu akishitakiwa ulidhalilisha jeshi la Polisi katika mtandao wa whatsapp.
Wakili wa Serikali Winifrida Sumawe aliwasilisha hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi mkuu Dk. Yohana Yongolo alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe 26/10/2016 eneo la Kigamboni.
Mshitakiwa anadaiwa kuidhalilisha jeshi la Polisi kwa kusambaza ujumbe uliosomeka
"“Natangaza ndoa na askari yeyote atakayejipendekeza kwangu siku hiyo ataolewa bila mahari.”
Baada ya kusomewa shitaka mtuhumiwa alikana shitaka hilo na upande wa mashitaka ulidai upelelezi haujakamilika.
Hakimu alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kila mmoja asaini bondi ya Sh1 milioni na kati ya wadhamini hao mmoja awe na mali isiyohamishika.

EmoticonEmoticon