Hatimae shirikisho la mpira nchini Tanzania limeyasikia malalamiko ya klabu ya Simba yaliyowasilishwa kwa Waziri kwa barua ambayo ikielezea matatizo yaliyopo katika uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya malalamiko hayo ni kwamba uwanja wa Uhuru si rafiki kwa wachezaji kwani raba zake zimechakaa na kusababisha wachezaji kuumia pindi wanapodondoka.
Pia uwanja haukidhi idadi ya mashabiki kwani mechi dhidi ya Azam mashabiki wengi walibaki nje kutokana na uwanja kujaa.
Kutokana na malalamiko hayo na mengine mengi TFF imehamishia michezo ijayo ya ligi kuu kwa timu zinazotumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wa Nyumbani na kuzihamishia uwanja wa Taifa mpaka ukarabati utakapofanyika katika uwanja wa Uhuru.

EmoticonEmoticon