YANGA YAMKODISHIA MANJI TIMU KWA MIAKA 10

6:30 AM
WANACHAMA wa Yanga wamekubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo.

Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika leo ukumbi wa Diamond jubilee, Dar es Salaam.

Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji. Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu, Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji. 

Manji aliwaambia wanachama hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati ya Utendaji na akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.

Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya watatu hao ambaye alikuwepo mkutanoni ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na kuondoka.

Mwanachama mwingine, Siza Lyimo ambaye Manji alitaka aondoke, yeye aliomba msamaha na wanachama wakamsamehe na Mwenyekiti huyo akabariki msamaha huo.

Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »