WEST HAMmUNITED YAFUNGUA UWANJA WAKE MPYA KWA USHINDI WA 3-0 KATIKA MECHI YA EUROPA HATUA YA MCHUJO.

3:39 PM

CHEIKHOU KOUYATE AWA WA KWANZA KUFUNGA UWANJA MPYA WA LONDON STADIUM

           Mfungaji wa goli la kwanza Cheikhou Kouyate
Timu ya West Ham United wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya timu ya NK Domzale katika mechi ya marudiano ya mchujo wa ligi ya Europa kuwania kupata nafasi ya kuingia kwenye hatua ya makundi.
Ikicheza kwa mara ya kwanza katika dimba lake jipya la London Stadium linalobeba watazamaji 54,000 Cheikhou Kouyate ilimchukua dakika 8 tu kuandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli katika uwanja huo.
Kouyate aiongeza goli la pili mnamo dakika ya 25 na kuifanya West ham iende mapumziko ikiwa inaongoza magoli 2-0
Dakika ya 81 Sofiane Feghouli aliifungia West Ham goli la tatu na kufanya jumla ya matokeo kuwa 4-2 baada ya mechi ya awali ambapo West Ham walifungwa magoli 2-1 ugenini.
 
West Ham inahitaji kushinda mechi moja mbele ili kufuzu kwenye hatua za makundi za ligi ya Europa na kuungana na Manchester United pamoja na Southmpton ambao walifuzu moja kwa moja.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »