Kikosi cha Brazil kilichocheza na Afrika ya kusini
Timu ya Taifa ya Olimpiki ya Brazi imeshindwa kutamba nyumbani mbele ya watoto wa kizuli (Afrika ya kusini) ambao kwa takribani dakika 30 za mwisho za mchezo walicheza pungufu ya mchezaji mmoja (Mothobi Mvala) aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea vibaya kiungo wa Brazil Zeca
Mounekano wa Neymer baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo
Matokeo hayo ya 0-0 yameonekana kuwaumiza na kuwachanganya wabrazil hao waliokuwa wanaongozwa na Neymer uwanjani.
Brazil inabidi ijilaumu yenyewe baada ya kukosa magoli kadhaa ya wazi. Mshambuliaji mpya wa Manchester City Gabrier Jesus almanusra aipatie Brazil goli lakini shuti lake liligonga mwamba wa goli la Afrika ya kusini.
Siamini! kweli tumewakosa? Huu ni mshangao anaoonekana kuwa nao Neymer baada ya kipyenga cha mwisho cha mchezo kupulizwa.
Neymer alionekana kuwa na wakati mgumu baada ya vijana wa ki south kujipanga vyema katika safu yao ya ulinzi na kuokoa hatari zote zilizoelekezwa langoni kwao.
Angalia Picha zaidi:-












EmoticonEmoticon