MAKAMU RAIS WA BARCELONA AIPONDA UEFA KWA KUWAACHA MESSI NA SUAREZ KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MCHEZAJI BORA ULAYA

4:41 AM
Makamu wa Rais wa Barcelona Jordi Mestre ameliambia shirikisho la soka la UEFA kuwa limejiingiza katika skendo baada ya kuwaondoa kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa Ulaya wachezaji wa Barcelana Messi na Suarez.
Mestre amedai ya kwamba takwimu ya viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji wa Barcelona Messi na Suarez  vinashinda vile vya Ronaldo na Balle wa Real Madrid na Griezmann wa Atletico Madrid ambao walitangazwa na UEFA kama wachezaji wa tatu wa mwisho watakaotoa mshindi katika kinyang'anyiro hicho.
Katika akaunti yake ya Twitter Bosi huyo wa Barcelona amenyesha Takwimu za magoli na assist baina ya wachezaji hao na kudai hapo UEFA wameongopa katika uteuzi wao na hiyo kwake anaichukulia kama ni shutuma kubwa kwa UEFA.
Ukiangalia chati hiyo utaona Messi na Suarez wamefunga magoli 107 na kutoa jumla ya assist 55, huku Ronaldo na Bale wakifunga magoli 78 na kutoa pasi za magoli  34, hapo utaona wazi nanai hasa anastahili kuwepo kwenye ushindani huo.
Mestre ameishutumu UEFA  na kwenda mbali kudai hajui vigezo gani wametumia katika uteuzi huo ambae kwake anasema ni wa upendeleo na ni kshfa kwa UEFA.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »