Wakati Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) likitangaza kuandaa mikutano ya hadhara kote nchini kwa siku moja, chama hicho kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu kitakachofanyika leo na kesho kujadili hali ya kisiasa nchini na njia za kuiimarisha kuanzia ngazi ya vitongoji.
Chadema imeitisha kikao hicho wakati kukiwa na taarifa kuwa, wanachama waliojiunga nacho wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita, wanatarajiwa kutangazwa kurejea CCM wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho unaofanyika leo mjini Dodoma.
Hadi jana majina ya wanachama hao wa Chadema wanaohamia CCM, yalikuwa hayajafahamika zaidi ya habari kuenea kuwa Mgana Msindai ni mmoja wao.
Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka alithibitisha, lakini hakutaja majina akisema wamepokea maombi mengi, lakini kesho ndiyo watayataja.
mwananchi
mwananchi

EmoticonEmoticon