Mama akamatwa na mirungi ‘Airport’

11:48 PM
Jeshi la Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania wakishirikiana na maafisa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wamemtia mbaroni mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Aziza Suleiman Ally (pichani), mkazi wa Mombasa Kwamchina, Zanzibar akiwa na mirungi.
Imeelezwa kuwa Aziza alinaswa uwanjani hapo Julai 13, mwa huu saa nane mchana akiwa ameficha mirungi hiyo sehemu mbalimbali ya mwili wake kama vile kwapani, kwenye matiti na sehemu za siri.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Maltin Otieno alisema ni kweli tukio hilo lilitokea.
Kamanda Otieno alisema kuwa Aziza alinaswa uwanjani hapo akiwa anajiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Msumbiji kwenda nchini humo akiwa ameficha mirungi mibichi pakiti nne sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Ni kweli sisi jeshi la polisi kwa kushirikiana na Usalama wa Taifa wa uwanjani hapa, tumemkamata Aziza Suleiman Ally (34) mkazi wa Mombasa Kwamchina Zanzibar raia wa hapa Tanzania akiwa na mirungi pakiti nne za uzito wa kilo nne akiwa amezificha sehemu mbalimbali za mwili,” alisema kamanda huyo.
Hata hivyo, alisema kuwa thamani ya mirungi hiyo bado haijajulikana na kutoa honyo kali kwa wale ambao wanajidanganya kutaka kupitisha madawa ya kulevya uwanjani hapo kwani ni lazima watakamatwa.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »