Didier Drogba amekuwa na historia nzuri ya kuifunga Arsenal pindi wanapokutana hususan katika kipindi Drogba alipokuwa akichezea Chelsea katika ligi kuu ya Uingereza. Lakini mara hii Drogba ameifunga tena Arsenal goli 1 katika mechi ambayo Arsenal waliibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya mastaa wanaokipiga katika ligi kuu ya Marekani.
Goli la Drogba linakuwa ni goli la 16 kuifunga Arsenal baada ya kufanya hivyo mara 15 kipindi anacheza ligi ya Uingereza.
Arsenal walipata goli dakika za mwanzo kwa mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Joel Campbell kabla ya Drogba kusawazisha.
Mfungaji wa goli la kwanza la Arsenal Joel Campbell
Goli lla pili la Asenal lilifungwa dakika za lala salama za mchezo na kinda Chba Akpom.




EmoticonEmoticon